Fahamu Kuhusu huduma ya kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba.
Na Abel Msumba, *Huduma ya Mobile Number portability (MNP) ina maana gani kwa mtumiaji* ? Huduma ya kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani (MNP), ina maana kuwa mtumiaji anabaki na namba yake ya awali iwapo ataamua kuhamia mtandao mwingine wa simu za kiganjani nchini Tanzania. Kimsingi, ni huduma ambayo inakuwezesha kubakia na namba yako bila kujali unatumia mtandao gani. Hivyo, iwapo utabadilisha mtoa huduma wa simu za kiganjani hutakuwa na haja ya kusumbuka kuwaataarifu watu wako wa karibu – marafiki, familia na wafanyakazi wenzako au washirika wako kwamba umebadilisha namba kwani inabakia ileile. Huduma ya MNP ina faida zipi? Utaendelea kutumia namba yako ya awali unapohama kutoka mtoa huduma mmoja kwenda mwingine na hivyo kufurahia uhuru na utulivu katika matumizi. Utapokea simu na meseji bila kujali ni mtandao upi umehamia na bila kuwa na haja ya kuwataarifu marafiki, familia na ...