Mashabiki Arsenal waamua kuuza tiketi zao

Mashabiki Arsenal waamua kuuza tiketi zao Msumbaabely BLOG / 

London, England.Maelfu ya mashabiki wa Arsenal waliokuwa na tiketi za mechi ya marudiano baina ya timu yao na Bayern Munich wameanza kuziuza tiketi hizo baada ya majanga waliyokutana nayo kwenye mechi ya kwanza.

Hakukuwa na tiketi yoyote kuhusu mechi hiyo ya Emirates zote zilikuwa zimekwishwa kabla ya mechi yao ya kwanza ya kipigo cha mabao 5-1 huko Allianz Arena, lakini sasa zimeanza kupatikana sokoni.

Kikosi hicho cha kocha Arsene Wenger kinahitaji kufanya maajabu kwenye mechi ya marudiano itakayofanyika Machi 7 ili kusonga mbele, lakini hata wale mashabiki wenye roho nguvu wa timu hiyo wanaamini hilo haliwezekani.

Kwa kipigo hicho, Arsenal sasa itakwama kuvuka hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya saba mfululizo. Baada ya awali uwanja wa Emirates kuonekana kuwa tiketi zote za mechi zimeuzwa, lakini sasa imefichuka kutakuwa na siti zitakazokuwa wazi kwa sababu mashabiki wa Arsenal wameamua kutafuta wateja wa kuwauzia kama itawakosa, basi kiti husika kitakuwa wazi hasa kwa jukwaa la Magharibi na lile jukwaa maarufu la North Bank lililonyuma ya goli.

Comments

Popular posts from this blog