Baadhi ya viongozi wa vijiji wamekamatwa kwa kuhamasisha wananchi kulima Bangi wilayani Muleba.

Baadhi ya viongozi wa vijiji wamekamatwa kwa kuhamasisha wananchi kulima Bangi wilayani Muleba.

Msumbaabely BLOG /

Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango amewakamata baadhi ya wenyeviti na watendaji wa serikali za vijiji walioshindwa kusimamia miradi ya maendeleo ya jamii kwa lengo la kunusuru janga la njaa na badara yake wamehamasisha wakulima kilimo cha zao haramu la bangi na kutumia mbolea ya kukuzia mazao ya chakula kwenye mimea ya dawa za kulevya kinyume cha sheria za nchi.

Watendaji hao wamekamatwa katika operesheni maalumu ya kudhibiti dawa za kulevya iliyohusisha kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera ambapo watu kumi wamekamatwa wakimiliki mashamba saba ya dawa za kulevya aina ya bangi katika kijiji cha Rwigembe kata ya Ngenge kwa kosa la kutumia mbolea ya serikali iliyotolewa kwa wakulima kusaidia kukuzia mahindi na badala yake mbolea hiyo imetumika kukuzia mimea haramu aina ya bangi kinyume cha sheria za nchi.

Baadhi ya wakulima wakabainisha kuwa soko la bangi katika wilaya ya Muleba limepanda kutoka shilingi laki moja hadi shilingi laki mbili kwa ndoo moja na kusema kwamba mawakala wamekuwa wakiwaletea mbegu na dawa za kuuwa wadudu na wanapovuna mawakala hufika mara moja kuchukua mzigo unaouzwa ndani na nje ya nchi.

Comments

Popular posts from this blog