https://youtu.be/K2O4BhXYwC8

HABARI ZA MASTAA


Roma Mkatoliki ajisajili rasmi BASATA

Leo April 05,2018 msanii wa Hip Hop Roma Mkatoliki amekutana na BASATA  tena ambapo safari hii amejisajili na kukabidhiwa cheti cha kutambulika na Baraza la sanaa Taifa (BASATA) kama msanii na hii ni baada ya kupewa sharti na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  ili aondolewe adhabu yake ya kufungiwa miezi sita.

March 1,2018 msanii Roma Mkatoliki alifungiwa kazi zake za sanaa na BASATA kwa miezi sita kutokana na wimbo wake wa “Kibamia” kutofuata maadili ya Kitanzania lakini March 29,2018 Roma Mkatoliki alitangaza rasmi kuufuta wimbo huo baada ya kupata msamaha wa Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dkt Harrison Mwakyembe

https://youtu.be/K2O4BhXYwC8

Comments